Prof. Rasel Madaha naye atakwepo kwenye siku ya wanaume wa kitanzania 2025

MUNGU atupiganie ili sote tuweze kushiriki kwenye tukio hili la kitaifa. Usipange kukosa karibuni sana. Tafadhali bofya [hapa]

Kuhusu jinsi ya kushiriki katika maazimisho ya siku ya mwanaume 2025, tafadhali bofya [hapa]

Kujua chimbiko la siku ya mwanaume wa kitanzania, tafadhali bofya [hapa]

Prof. Madaha anakukaribisha sana katika maazimisho hayo.

Maazimisho ya siku ya wanaume wa kitanzania mwaka 2025

AGEN kwa kushirikana na Asasi ya maendeleo ya jamii (CDA) ya wanachuo wa Sokoine University of Agriculture (SUA) wanaosoma shahada ya maendeleo ya jamii na ugani tuna kukaribisha katika maadhimisho ya Siku ya Mwanaume wa Kitanzania, yatakayofanyika tarehe 23/4/2025 katika viwanja vya shule ya msingi K/ndege, Morogoro, mjini.

Kila mwaka tarehe *23 Aprili*, Watanzania huja pamoja kusherehekea Siku ya Wanaume wa Kitanzania. Siku hii inalenga kuongeza uelewa na kutetea haki za wanaume na pia kuwafanya wawajibike kama wanaume wa Kitanzania.

Kaulimbiu ya mwaka 2025 ni *”MWANAUME WA KITANZANIA, MKOMBOZI WA JAMII NA CHACHU YA MABADILIKO”*

Tukio hili limeandaliwa na *Community Development Association* (CDA: https://www.coa.sua.ac.tz/extension/students/community-development-association-cda) na *Affirmative action on Gender Equality Network* (AGEN: https://www.agentz.org), ambapo *Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine* (SUA: https://www.sua.ac.tz/) na wanachuo kutoka chuo hicho ni miongoni wa wadau.

Tunawaalika Mashirika yasiyo ya kiserikali, watetezi wa haki za binadamu, Mashirika ya kiJamii, Vyombo vya Habari, Makampuni binafsi, na watu wengine wote wenye nia njema ili kufanikisha tukio hili.

Lengo kuu la maadhimisho haya ni kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusu mchango wa mwanaume wa kitanzania katika maendeleo ya familia, jamii, na taifa kwa ujumla. Pia, yatahusisha mijadala, mafunzo, na shughuli za kijamii zinazolenga kuinua hadhi ya mwanaume na kumhamasisha katika kuleta maendeleo chanya.

Kwa kutambua umuhimu wa ushirikiano wako wadau mbalimbali tuna wakaribisha kutoa michango yao kupitia taratibu zifuatazo:

  • Msaada wa kifedha kusaidia maandalizi na gharama za tukio.
  • Kutoa bidhaa au huduma zinazohitajika kwa ajili ya tukio.
  • Ushirikiano wa kimkakati katika uhamasishaji na utoaji wa elimu kwa jamii.

Tunaamini ushiriki wa wadau utasaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha malengo ya maadhimisho haya, huku pia wakipata fursa ya kutangaza shughuli na huduma zako kwa jamii na wageni waalikwa wapatao zaidi ya watanzania 1500.

Unaweza kutuma mchango wako katika benki ya:

Jina la benki: MKOMBOZI BANK

Jina la akaunti: AFFEMATIVE ACTION ON GENDER EQUALITY NETWORK (AGEN)

Namba ya Akaunti: 00711509115301

Muhimu: Unapochangia, tafadhali elezea kuwa mchango huo ni wa siku ya mwanaume wa kitanzania

Vipaumbele Vya Wadhamini Katika Maadhimisho Ya Siku Ya Mwanaume Wa Kitanzania

Katika kuthamini mchango wa wadhamini wetu, tumetengeneza viwango vya udhamini vinavyotoa nafasi ya kutangaza na kutambua mchango wa kila mdhamini kulingana na kiwango cha msaada wao. Vifuatavyo ni orodha ya vipaumbele kwa kila kiwango cha udhamini:

1. Gold Sponsor – TZS 1,000,000 Na Zaidi

  • Kutangazwa kama mdhamini mkuu wa maadhimisho.
  • Nembo ya kampuni/taasisi kuwekwa kwenye mabango, fulana, vipeperushi, na nyaraka rasmi za tukio.
  • Nafasi ya kutoa hotuba fupi katika tukio.
  • Kutangazwa kwenye vyombo vya habari (TV, redio, na mitandao ya kijamii) kama mdhamini mkuu.
  •  Nafasi ya kuonyesha na kuuza bidhaa au huduma kwenye banda maalum.
  • Tiketi 5 za VIP kwa wawakilishi wa mdhamini.

2. Silver Sponsor – TZS 500,000

  • Kutangazwa kama mdhamini mshiriki wa maadhimisho.
  • Nembo ya kampuni/taasisi kuwekwa kwenye mabango na nyaraka za tukio.
  • Kutangazwa kwenye mitandao ya kijamii ya maadhimisho.
  • Nafasi ya kuonyesha bidhaa au huduma kwenye banda la kawaida.
  • Tiketi 3 za VIP kwa wawakilishi wa mdhamini.

3. Iron Sponsor – TZS 200,000

  • Kutajwa kama mdhamini katika maadhimisho.
  • Nembo ya kampuni kuwekwa kwenye mabango madogo ya tukio.
  • Kutangazwa kwenye mitandao ya kijamii ya maadhimisho.
  • Tiketi 2 za kawaida kwa wawakilishi wa mdhamini.

Tunathamini mchango wa kila mdau na tunaamini kwamba ushirikiano huu utakuwa wa manufaa kwa pande zote. Karibu tushirikiane kufanikisha tukio hili muhimu!

Endapo ungependa kushiriki nasi kama shirika au mwananchi wa kawaida, tafadhali wasiliana nasi kupitia taarifa zifuatazo:

πŸ‘‡πŸΏ

1. Mariam Yahaya Msigala (Mkurugenzi wa Maazimisho) kwa namba ifuatayo +255617735221 au barua pepe inquiries@agentz.org

2. Aisha Mohamed Kikala (Mkurugenzi Msaidizi wa Maazimisho) kwa namba ifuatayo +255656782627 au barua pepe inquiries@agentz.org

3. George Elisha (Mratibu wa wahitimu) kwa namba ifuatayo +255616549017 au barua pepe inquiries@agentz.org

4. Prof. R. Madaha (Mkurugenzi wa shirika na mlezi) kupitia barua pepe zifuatazo rasel.madaha@agentz.org and rasel.madaha@sua.ac.tz

Waanzilishi wa kuazimisha Siku ya Wanaume wa Kitanzania walikuwa ni wanafunzi kutoka *Idara ya Ugani na Maendeleo ya Jamii* (DAECD: https://www.coa.sua.ac.tz/extension/#) katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), shirika la Affirmative action on Gender Equality Network (AGEN), mashirika yasiyo ya kiserikali, na Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs). Tukio hilo lime kuwa tukio la kitaifa lenye mvuto kutoka Kwa wadau mbalimbali kutoka ulimwenguni kote πŸŒŽπŸŒ.

πŸ“’πŸ“’πŸ“’πŸ“’_*Sambaza habari*_ πŸ“’πŸ“’πŸ“’πŸ“’

*Sekretarieti ya Maandalizi ya Tukio*

Mwanaume wa kitanzania ni mwanaume wa kitanzania na hafanani na wanaume wengine. Ili kujua chanzo na historia ya maazisho ya siku ya mwanaume wa kitanzania tafadhali bofya katika kiunganishi kifuatacho https://www.agentz.org/index.php/siku-ya-mwanaume-wa-kitanzania/ au bofya [hapa]

πŸ“’πŸ“’πŸ“’πŸ“’_*Sambaza habari kila pande*_ πŸ“’πŸ“’πŸ“’πŸ“’

Invitation to Participate in the Tanzanian Men’s Day on 23rd April 2025

Every year on the *23rd of April*, Tanzanians come together to celebrate Tanzanian Men’s Day. This day aims at raising awareness and advocating for men’s rights as well as making them take their responsibility as Tanzanian men. 

The event is organized by the *Community Development Association* (CDA: https://www.coa.sua.ac.tz/extension/students/community-development-association-cda) and the *Affirmative action on Gender Equality Network* (AGEN: https://www.agentz.org), with significant support from *Sokoine University of Agriculture* (SUA: https://www.sua.ac.tz/). 

We would like to invite *collaborations* from Gender-Aware Organizations, community-Based Organizations, the Media, and other like-minded individuals who are interested in supporting this event and contributing to its success.

If you would like to express your interest, whether as an organization or an individual, please reach out to the contacts provided below:

πŸ‘‡πŸΏ

1. Mariam Yahaya Msigala (Event Director) at +255617735221

2. Aisha Mohamed Kikala (Deputy Event Director) at +255656782627

3. George Elisha (Event Alumni Coordinator) at +255616549017

4. Prof. R. Madaha (Chaplain) via rasel.madaha@agentz.org and rasel.madaha@sua.ac.tz

The pioneers of the Tanzanian Men’s Day were students from the *Department of Agricultural Extension and Community Development* (DAECD: https://www.coa.sua.ac.tz/extension/#) at Sokoine University of Agriculture (SUA), Affirmative action on Gender Equality Network (AGEN) members of NGOs, and Local Government Authorities (LGAs) in Morogoro. The event has been rebranded to become a national event attracting interest from across the world πŸŒŽπŸŒ.

Event Organizing Secretariat

If you would like to get details, please click hereΒ