

Wanaume na wanawake wa Tanzania, tunawaalika mshiriki nasi katika maadhimisho haya muhimu ya kitaifa kwa kujiunga na kundi letu la WhatsApp kupitia kiunganishi hiki: https://chat.whatsapp.com/B5bv3xzUd8DGHTR0oGGBhe?mode=git au bofya hapa. (Kundi hili ni Kwa wale tu waliothibitisha kushiriki).

Lengo letu ni kuhakikisha kila Mtanzania anashiriki kikamilifu na kutoa mchango wake. Hakuna kiwango maalum cha mchango—unaweza kuchangia kiasi chochote kulingana na uwezo wako na ukishindwa bado unakaribishwa kuja Morogoro. Mchakato huu ni shirikishi na tutaamua tunasherekea Kwa namna ghani.
Tukio hili litafanyika ndani ya ukumbi (indoor event), hivyo hali ya hewa haitakuwa kikwazo. Tutatafuta ukumbi kulingana na mwitikio. Tafadhali thibitisha ushiriki wako kabla ya tarehe 11 April 2026.
Sambamba na tukio la jumla Kwa kila mtu, kutakuwepo na kongamano la kitaaluma pia. Hivyo, kwa wale wanaotamani kushiriki katika kongamano la kitaaluma katika ukumbu wa ICE, SUA, ada ya ushiriki ni Tshs 100,000 kwa siku yaani tarehe 22 April (ni 100,000) na 23 April (ni 100,000). Uko huru kushiriki siku moja au zaidi kulingana na nafasi yako.
Jiunge sasa, tuwe pamoja kuenzi na kusherehekea Maadhimisho ya Siku ya Mwanaume wa Kitanzania.
🔥🔥🔥🔥🔥Changia kiasi chochote kupitia Yas Lipa number 45884820 Kwa ushiriki wa jumla na 100,000 Kwa kongamano la kitaaluma.

Zimebaki siku 24 tu!
Tunakaribia kuadhimisha Siku ya Mwanaume wa Kitanzania — siku ya mshikamano, heshima na kujenga kizazi cha wanaume bora wanaoenzi utamaduni na maadili ya taifa letu.
Mambo ya Msingi Tunayoangazia
Tunajenga Nini?
Mwanaume bora wa Kitanzania ni:
Wito wa Kampeni
Jiunge nasi katika safari hii ya kujenga kizazi cha wanaume bora.
Shiriki mijadala, semina na matukio ya kijamii.
Kumbuka: mwanaume bora hajengwi kwa maneno pekee, bali kwa vitendo thabiti na mshikamano wa kitaifa.
Kumbuka: Siku ya Mwanaume wa Kitanzania ni jukwaa la mshikamano na maendeleo. Tushirikiane, tuimarishe familia, jamii na taifa.
Chanzo cha taarifa: Sera mbalimbali za serikali*
Siku 29 Kabla ya Siku ya Wanaume Tanzania – Kukuza Ubunifu na Ujuzi wa Kazi kwa Vijana

Methali ya Kiswahili husema “Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo”. Ili kujenga kizazi cha wanaume wa Kitanzania wenye utu, heshima na mchango halisi kwa taifa, tunahitaji mikakati ya kukuza ubunifu na ujuzi wa kazi kwa vijana wa kike na kiume. Leo tunaangazia hatua, mkakati na mbinu za kitaifa zinazojengwa juu ya Katiba ya Tanzania, sera za utamaduni, na teknolojia za kisasa.
Hatua: Vijana Kufundishwa Stadi za Kazi Halali na Ubunifu
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977, kila mtu ana haki ya kufanya kazi na kupata malipo ya haki (Ibara ya 22–23), na pia haki ya kujielimisha na kujifunza stadi za maisha (Ibara ya 11). Hii inatoa msingi wa:
Mkakati: Kuendeleza Mafunzo ya Ufundi na Teknolojia ya Kisasa Sambamba na ya Jadi
Sera ya Utamaduni ya Tanzania (1997) inatambua umuhimu wa kuendeleza maarifa ya jadi pamoja na teknolojia mpya. Mafunzo haya yanajumuisha:
Kwa kuunganisha maarifa ya jadi na ya kisasa, tunajenga kizazi cha vijana wanaume wenye uwezo wa kuleta mabadiliko ya kiuchumi na kijamii.
Mbinu: Kuanzisha Vituo vya Ubunifu Vijijini na Mijini Vinavyoshirikisha Jamii
Katiba (Ibara ya 8) inasisitiza kuwa serikali ni ya watu na inalenga ustawi wa jamii. Vituo vya ubunifu vinavyoshirikisha jamii vinaweza:
Kwa kutumia teknolojia hizi, vijana wanapata maarifa, mitandao na fursa za kuendeleza ubunifu wao kwa njia jumuishi.
Hitimisho
Kukuza ubunifu na ujuzi wa kazi kwa vijana wa Kitanzania ni msingi wa:
Kwa kufanya hivyo, tunaunda kizazi cha wanaume wa Kitanzania wanaosimama kama nguzo za utu, ubunifu na maendeleo ya taifa.
Chanzo cha taarifa: Sera ya Utamaduni ya Tanzania ya mwaka 1997 na sera nyingine

Utangulizi
Ikiwa imebakia siku 42, Leo tunaangazia sifa za mwanamke wa kitanzania anaye enzi utamaduni wa kitanzania. Awali ya yote, Methali za Kiswahili husema: “Kuzaa si kazi, kazi ni kulea” na “Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo”. Methali hizi hazimhusu mwanaume pekee, bali pia mwanamke ambaye ndiye nguzo ya familia na jamii. Katika kizazi kipya, wanawake wa Kitanzania wanabeba jukumu kubwa la kuendeleza utamaduni, kuhimiza mshikamano na kuleta maendeleo bila kupoteza utambulisho wa taifa.
Asubuhi ya Mwanamke Bora – Neema
Neema ni kijana wa Kitanzania anayejiendeleza katika fani ya ualimu wa Kiswahili na historia. Anaamka mapema, akianza siku yake kwa sala na maandalizi ya familia. Huwahimiza watoto wa jirani kusoma na kuheshimu wazee, akitambua kuwa malezi bora ndiyo msingi wa kizazi chenye maadili.
Kazini na Elimu
Kazini, Neema ni mwalimu anayejivunia kutumia Kiswahili kama lugha ya kufundishia. Hupitisha maarifa ya historia na mila za taifa kwa wanafunzi wake, akiwafundisha methali, nyimbo za jadi na fasihi simulizi. Anaamini kuwa elimu ni sehemu ya utamaduni na haiwezi kutenganishwa na maadili ya jamii .
Jamii na Ushirikiano
Katika kijiji chake, Neema ni kiongozi wa kikundi cha wanawake. Hupinga mila mbaya kama unyanyasaji wa kijinsia na ubaguzi, huku akihimiza usawa wa kijinsia na mshikamano wa kijamii. Hushirikiana na wanaume na wanawake kwa pamoja katika miradi ya maendeleo, akisisitiza mshikikano bila kujali jinsi, dini, umri au rangi . Yeye huthamini na kutambua mchango chanya wa mwanaume katika familia, Jamii, na taifa.
Burudani na Utamaduni
Jioni, Neema hushiriki katika vikundi vya sanaa za maonyesho. Hupiga ngoma za jadi, kuimba nyimbo za Kiswahili na kushiriki tamthiliya zinazofundisha maadili. Huhimiza vijana wenzie kuenzi urithi wa taifa, huku akiwahimiza kutumia teknolojia ya kisasa kwa ubunifu bila kupoteza utambulisho wa Kitanzania.
Hitimisho
Hadithi ya Neema ni taswira ya mwanamke bora wa Kitanzania katika kizazi kipya: mlezi wa familia, mzalendo wa taifa, mlinzi wa urithi wa utamaduni, na kiongozi wa kijamii. Anaishi kwa misingi ya methali na mwongozo wa Sera ya Utamaduni, akijenga kizazi kinachoweza kushindana kimataifa bila kupoteza mshikamano na utambulisho wa taifa.
Chanzo cha simulizi: Sera ya Utamaduni ya Tanzania ya mwaka 2007

Utangulizi
Methali za Kiswahili hufundisha hekima ya malezi na maadili ya jamii. Methali ya “Kuzaa si kazi, kazi ni kulea” hutufundisha kuwa jukumu kubwa la mzazi si tu kumleta mtoto duniani bali kumkuza kwa maadili mema. Vilevile methali ya “Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo” inatufundisha kuwa malezi na utamaduni wa jamii ndiyo msingi wa tabia na utu wa mtu. Hivyo basi, mwanaume bora wa Kitanzania ni yule anayejengwa na kulelewa katika misingi ya utamaduni wake, na baadaye kuishi kwa kuenzi na kuendeleza mila, desturi, na maadili ya taifa lake.
Tabia na Sifa Kuu za mwanaume wa kitanzania anayethamini utamaduni wa kitanzania
Hitimisho
Mwanaume bora wa Kitanzania ni kielelezo cha utamaduni wake. Ni mlezi, mzalendo, mwenye nidhamu na heshima, mlinzi wa familia na mazingira, na mzalishaji wa maendeleo kupitia elimu na kazi halali. Kwa kuishi kwa misingi ya methali “Kuzaa si kazi, kazi ni kulea” na “Mtoto umleavyo ndivyo akuavyo”, mwanaume huyu hujenga kizazi chenye maadili, mshikamano na utambulisho wa taifa.
Chanzo: sera ya utamaduni ya Tanzania ya mwaka 1997

Utangulizi
Maadili ya mwanaume wa Kitanzania ni mwongozo wa kimaadili, kijamii na kiutamaduni unaojengwa juu ya misingi ya historia, sera na dira za taifa. Yanalenga kumtengeneza mwanaume mwenye utu, mshikamano, uzalendo na uwajibikaji katika familia, jamii na taifa. Kupitia nyaraka mbalimbali za kitaifa — Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050, Sera ya Utamaduni, Sera ya Maendeleo ya Jamii (Community Development Policy), Wimbo wa Taifa, na Sera ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake 2023 — tunapata taswira ya mwanaume bora wa Kitanzania anayejali utu, usawa wa kijinsia, maendeleo endelevu na mshikamano wa kitaifa.
Hapa chini tumekusanya jumla ya maadili 40 ya mwanaume wa Kitanzania.
🏅 Maadili ya Mwanaume wa Kitanzania
Kutoka Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2050
Kutoka Sera ya Utamaduni
Kutoka Sera ya Maendeleo ya Jamii ya (Community Development Policy) (1996)
Kutoka Wimbo wa Taifa
Kutoka Sera ya Jinsia na Maendeleo ya Wanawake 2023
✨ Hitimisho
Maadili haya 40 yanamjenga mwanaume wa Kitanzania kama mzalendo, mwenye heshima, mlinzi wa familia na taifa, mtetezi wa haki za binadamu, na mshiriki wa maendeleo jumuishi. Yanaunganisha historia ya taifa, sera za kijamii na utamaduni, pamoja na dira ya maendeleo ya 2050, ili kuunda taswira ya mwanaume bora anayechangia katika ustawi wa taifa na kizazi kijacho.
Kwa taarifa zaidi tembelea 👉🏿 https://www.agentz.org/index.php/2026/03/07/kuelekea-maazimisho-ya-siku-ya-mwanaume-wa-kitanzania-23-april-2026/ (au bofya hapa)

Bado siku 47 kufikia kilele cha Maadhimisho ya Siku ya mwanaume wa kitanzania.
1. Kujua zaidi kuhusu mchango wa mwanaume wa kitanzania tembelea
https://youtu.be/NVa6Zd8PkS8?si=KsWEfMWO5BVerUQx (au bofya hapa)
2. Kupata taarifa zaidi kuhusu tukio letu tembelea
https://www.agentz.org/index.php/conferences/ (au bofya hapa)
3. Kushiriki katika kuandaa Agenda ya Mwanaume wa Kitanzania 2026. Tafadhali jaza dodoso la kielekroniki hapa
https://forms.gle/AgusMn9Z7JwFSXax8 (au bofya hapa)
4. Ukitaka kujua zaidi Kwa Nini tunamwazimisha mwanaume wa kitanzania, tafadhali tembelea link ifuatayo
https://www.agentz.org/index.php/the-tanzanian-man/ (au bofya hapa)
4. Mada ya tarehe 6/3/2026, ijumaa, ni kuhusu Maadili ya mwanaume wa kitanzania. Tutasambaza link yenye video punde
5. Mada ijayo tarehe 13/03/2026 ni Mchango wa Mwanaume wa Kitanzania katika ujenzi wa utamaduni wa kitanzania
Motto: The Tanzanian Man: Guardian of DIGNITY, Builder of Strong Families, and Light of National Development
Kauli Mbiu: Mwanaume wa Kitanzania: Mlinzi wa UTU, Mjenzi wa Familia Imara na Mwanga wa Maendeleo ya Taifa
Mjadala katika video unapatikana katika kiunganishi kifuatacho 👇🏿
https://youtu.be/NVa6Zd8PkS8?si=KsWEfMWO5BVerUQx au bofya [hapa]
Ujenzi wa familia imara ni msingi wa ustawi wa jamii na taifa. Mwanaume ana nafasi ya kipekee katika mchakato huu, na mchango wake hujidhihirisha katika nyanja kadhaa:
Ndani ya Familia

Katika Jamii

Katika Taifa
Muunganiko wa Familia, Jamii na Taifa
Familia imara huzaa jamii yenye mshikamano, na jamii imara hujenga taifa lenye nguvu. Mwanaume, kama mhimili wa familia, anaposhiriki kikamilifu katika malezi, uchumi na uongozi, mchango wake huenea hadi ngazi ya kijamii na kitaifa.
Kwa maneno mengine: Baba bora hujenga Familia bora inayopelekea kuwa Jamii bora na hatimaye Taifa bora.
Tembelea tovuti ili kupata taarifa zaidi: https://www.agentz.org/index.php/conferences/
Angalia video ya mada hapa

Utangulizi
Karibu kwenye Dodoso la Kuandaa Ajenda ya Mwanaume wa Kitanzania 2026.
Siku ya Mwanaume wa Kitanzania (Aprili 23) ni jukwaa la kitaifa linalolenga kutafakari nafasi ya wanaume katika familia, jamii na taifa. Kupitia fomu hii, tunakusanya maoni na mawazo yako ili kuunda Ajenda ya Mwaka 2026, ambayo itasaidia kuimarisha mshikamano wa kijamii, usawa wa kijinsia, na maendeleo endelevu ya taifa letu.
Ajenda hii inalenga:
Familia na Malezi: Kuimarisha jukumu la wanaume katika malezi na ustawi wa familia.
Uwezeshaji Kiuchumi: Kuwezesha wanaume kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kisasa sambamba na wanawake.
Afya na Ustawi: Kuboresha afya ya wanaume, ikiwemo afya ya akili, uzazi na kupunguza changamoto za kiafya.
Uongozi na Jamii: Kuongeza uwajibikaji wa wanaume katika uongozi, maamuzi na mshikamano wa kijamii.
Teknolojia na Ubunifu: Kuhakikisha wanaume wanatumia TEHAMA na ubunifu kwa maendeleo ya familia na taifa.
Usawa na Haki za Kijinsia: Kupunguza ukatili wa kijinsia na kukuza usawa wa kijinsia kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Jinsia 2023.
Dira ya Taifa 2050: Kuchangia katika malengo ya taifa ya uchumi jumuishi, maendeleo ya kijamii na ustawi wa mazingira.
Ushiriki wako ni muhimu katika kuunda mustakabali wa wanaume wa Kitanzania. Tafadhali jibu maswali kwa uaminifu na kwa mtazamo wako binafsi. Tafadhali bonyeza [hapa] kujaza dodoso.