
AGEN kwa kushirikana na Asasi ya maendeleo ya jamii (CDA) ya wanachuo wa Sokoine University of Agriculture (SUA) wanaosoma shahada ya maendeleo ya jamii na ugani tuna kukaribisha katika maadhimisho ya Siku ya Mwanaume wa Kitanzania, yatakayofanyika tarehe 23/4/2025 katika viwanja vya shule ya msingi K/ndege, Morogoro, mjini.

Kila mwaka tarehe *23 Aprili*, Watanzania huja pamoja kusherehekea Siku ya Wanaume wa Kitanzania. Siku hii inalenga kuongeza uelewa na kutetea haki za wanaume na pia kuwafanya wawajibike kama wanaume wa Kitanzania.
Kaulimbiu ya mwaka 2025 ni *”MWANAUME WA KITANZANIA, MKOMBOZI WA JAMII NA CHACHU YA MABADILIKO”*
Tukio hili limeandaliwa na *Community Development Association* (CDA: https://www.coa.sua.ac.tz/extension/students/community-development-association-cda) na *Affirmative action on Gender Equality Network* (AGEN: https://www.agentz.org), ambapo *Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine* (SUA: https://www.sua.ac.tz/) na wanachuo kutoka chuo hicho ni miongoni wa wadau.

Tunawaalika Mashirika yasiyo ya kiserikali, watetezi wa haki za binadamu, Mashirika ya kiJamii, Vyombo vya Habari, Makampuni binafsi, na watu wengine wote wenye nia njema ili kufanikisha tukio hili.
Lengo kuu la maadhimisho haya ni kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusu mchango wa mwanaume wa kitanzania katika maendeleo ya familia, jamii, na taifa kwa ujumla. Pia, yatahusisha mijadala, mafunzo, na shughuli za kijamii zinazolenga kuinua hadhi ya mwanaume na kumhamasisha katika kuleta maendeleo chanya.
Kwa kutambua umuhimu wa ushirikiano wako wadau mbalimbali tuna wakaribisha kutoa michango yao kupitia taratibu zifuatazo:
- Msaada wa kifedha kusaidia maandalizi na gharama za tukio.
- Kutoa bidhaa au huduma zinazohitajika kwa ajili ya tukio.
- Ushirikiano wa kimkakati katika uhamasishaji na utoaji wa elimu kwa jamii.
Tunaamini ushiriki wa wadau utasaidia kwa kiasi kikubwa kufanikisha malengo ya maadhimisho haya, huku pia wakipata fursa ya kutangaza shughuli na huduma zako kwa jamii na wageni waalikwa wapatao zaidi ya watanzania 1500.
Unaweza kutuma mchango wako katika benki ya:
Jina la benki: MKOMBOZI BANK
Jina la akaunti: AFFEMATIVE ACTION ON GENDER EQUALITY NETWORK (AGEN)
Namba ya Akaunti: 00711509115301
Muhimu: Unapochangia, tafadhali elezea kuwa mchango huo ni wa siku ya mwanaume wa kitanzania
Vipaumbele Vya Wadhamini Katika Maadhimisho Ya Siku Ya Mwanaume Wa Kitanzania
Katika kuthamini mchango wa wadhamini wetu, tumetengeneza viwango vya udhamini vinavyotoa nafasi ya kutangaza na kutambua mchango wa kila mdhamini kulingana na kiwango cha msaada wao. Vifuatavyo ni orodha ya vipaumbele kwa kila kiwango cha udhamini:
1. Gold Sponsor – TZS 1,000,000 Na Zaidi
- Kutangazwa kama mdhamini mkuu wa maadhimisho.
- Nembo ya kampuni/taasisi kuwekwa kwenye mabango, fulana, vipeperushi, na nyaraka rasmi za tukio.
- Nafasi ya kutoa hotuba fupi katika tukio.
- Kutangazwa kwenye vyombo vya habari (TV, redio, na mitandao ya kijamii) kama mdhamini mkuu.
- Nafasi ya kuonyesha na kuuza bidhaa au huduma kwenye banda maalum.
- Tiketi 5 za VIP kwa wawakilishi wa mdhamini.
2. Silver Sponsor – TZS 500,000
- Kutangazwa kama mdhamini mshiriki wa maadhimisho.
- Nembo ya kampuni/taasisi kuwekwa kwenye mabango na nyaraka za tukio.
- Kutangazwa kwenye mitandao ya kijamii ya maadhimisho.
- Nafasi ya kuonyesha bidhaa au huduma kwenye banda la kawaida.
- Tiketi 3 za VIP kwa wawakilishi wa mdhamini.
3. Iron Sponsor – TZS 200,000
- Kutajwa kama mdhamini katika maadhimisho.
- Nembo ya kampuni kuwekwa kwenye mabango madogo ya tukio.
- Kutangazwa kwenye mitandao ya kijamii ya maadhimisho.
- Tiketi 2 za kawaida kwa wawakilishi wa mdhamini.
Tunathamini mchango wa kila mdau na tunaamini kwamba ushirikiano huu utakuwa wa manufaa kwa pande zote. Karibu tushirikiane kufanikisha tukio hili muhimu!
Endapo ungependa kushiriki nasi kama shirika au mwananchi wa kawaida, tafadhali wasiliana nasi kupitia taarifa zifuatazo:

1. Mariam Yahaya Msigala (Mkurugenzi wa Maazimisho) kwa namba ifuatayo +255617735221 au barua pepe inquiries@agentz.org
2. Aisha Mohamed Kikala (Mkurugenzi Msaidizi wa Maazimisho) kwa namba ifuatayo +255656782627 au barua pepe inquiries@agentz.org
3. George Elisha (Mratibu wa wahitimu) kwa namba ifuatayo +255616549017 au barua pepe inquiries@agentz.org
4. Prof. R. Madaha (Mkurugenzi wa shirika na mlezi) kupitia barua pepe zifuatazo rasel.madaha@agentz.org and rasel.madaha@sua.ac.tz
Waanzilishi wa kuazimisha Siku ya Wanaume wa Kitanzania walikuwa ni wanafunzi kutoka *Idara ya Ugani na Maendeleo ya Jamii* (DAECD: https://www.coa.sua.ac.tz/extension/#) katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), shirika la Affirmative action on Gender Equality Network (AGEN), mashirika yasiyo ya kiserikali, na Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs). Tukio hilo lime kuwa tukio la kitaifa lenye mvuto kutoka Kwa wadau mbalimbali kutoka ulimwenguni kote .
_*Sambaza habari*_
*Sekretarieti ya Maandalizi ya Tukio*

Mwanaume wa kitanzania ni mwanaume wa kitanzania na hafanani na wanaume wengine. Ili kujua chanzo na historia ya maazisho ya siku ya mwanaume wa kitanzania tafadhali bofya katika kiunganishi kifuatacho https://www.agentz.org/index.php/siku-ya-mwanaume-wa-kitanzania/ au bofya [hapa]
_*Sambaza habari kila pande*_