
Utangulizi
Karibu kwenye Dodoso la Kuandaa Ajenda ya Mwanaume wa Kitanzania 2026.
Siku ya Mwanaume wa Kitanzania (Aprili 23) ni jukwaa la kitaifa linalolenga kutafakari nafasi ya wanaume katika familia, jamii na taifa. Kupitia fomu hii, tunakusanya maoni na mawazo yako ili kuunda Ajenda ya Mwaka 2026, ambayo itasaidia kuimarisha mshikamano wa kijamii, usawa wa kijinsia, na maendeleo endelevu ya taifa letu.
Ajenda hii inalenga:
Familia na Malezi: Kuimarisha jukumu la wanaume katika malezi na ustawi wa familia.
Uwezeshaji Kiuchumi: Kuwezesha wanaume kushiriki kikamilifu katika uchumi wa kisasa sambamba na wanawake.
Afya na Ustawi: Kuboresha afya ya wanaume, ikiwemo afya ya akili, uzazi na kupunguza changamoto za kiafya.
Uongozi na Jamii: Kuongeza uwajibikaji wa wanaume katika uongozi, maamuzi na mshikamano wa kijamii.
Teknolojia na Ubunifu: Kuhakikisha wanaume wanatumia TEHAMA na ubunifu kwa maendeleo ya familia na taifa.
Usawa na Haki za Kijinsia: Kupunguza ukatili wa kijinsia na kukuza usawa wa kijinsia kwa mujibu wa Sera ya Taifa ya Jinsia 2023.
Dira ya Taifa 2050: Kuchangia katika malengo ya taifa ya uchumi jumuishi, maendeleo ya kijamii na ustawi wa mazingira.
Ushiriki wako ni muhimu katika kuunda mustakabali wa wanaume wa Kitanzania. Tafadhali jibu maswali kwa uaminifu na kwa mtazamo wako binafsi. Tafadhali bonyeza [hapa] kujaza dodoso.
Leave a Reply